Welcome to Bilal Muslim Mission of Tanzania (Charitable Organization)
CALL US NOW +255 745 111 150
DONATE NOW

MILAD-UN-NABI HAWZATU BILAL

Alhamdullillah, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) imefanikiwa kufanya Sherehe Maalumu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kipenzi chetu, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Ustadh Haji akifungua Maulid kwa kisomo cha Qur-an

Sherehe hizo zimefanyika Hawzatu Bilal, Temeke Dar es salaam na kuhudhuriwa na wakuu wa bodi, Mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akituma mwakilishi wake, Madrasa mbalimbali zikiwemo Madrasatul Mukhliswina, Madrasatul Aqswa, Madrasatul Azhar Sharif, Madrasatul Minhaj Twalibin, Madrasatul Saqina ambao walishiriki moja kwa moja ikiwa pamoja na usomaji wa milango.

Sehemu ya wahudhuriaji pia ilitokana na waumini wangine wake kwa waume kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na maeneo ya jirani. Sherehe hizi ni za kawaida na zinafanywa na watu mbalimbali kutoka jamii ya Kiislamu, malengo ikiwa kuzitaja sifa za mtukufu Mtume (s.a.w.w) na kutoa fursa kwa waumini wa kiislamu kuyatafakari maisha na matendo ya bwana mtume (s.a.w.w) na kisha kuyaingiza katika maisha yetu ya kila siku.

Hata hivyo Sherehe hizi zimefanyika kwa mara ya kwanza Hawzatu Bilal, hivyo zimetoa funzo kutokana na changamoto kadhaa zilizojitokeza, tunatarajia sherehe hizi kuwa bora zaidi kwa miaka ijayo. Kwa upekee tunatoa shukrani kwa wote walioacha shuguli zao na kushiriki kwenye tukio hili kubwa kabisa na pia shukrani za dhati kwa wahisani waliotushika mkono na kufanikisha kufanyika kwa shuguli hii kupitia michango yao mbalimbali…

CHINI: SEHEMU YA MATUKIO YA MAULID KWA PICHA

Ustadh Haji akifungua Maulid kwa kisomo cha Qur-an

Ndugu Hafidh Mansoor (Afisa Mtendaji Mkuu BMMT) akikaribisha na kuwatambulisha wageni

Sehemu ya waumini wanawake wakifuatilia Maulid kupitia projector…

Sehemu ya waumini wanaume walioshiriki kwenye maulid

Moja ya Madrasa (wageni waalikwa) walioshiriki kwenye Maulid

Sheikh Jabir Chandoo akiwasilisha mada wakati wa sherehe za Maulid

Sheikh Habib Mbota, Mshehereshaji (MC) akifuatilia kwa umakini sherehe za maulid

Jukwaa kuu likiwa na viongozi wa bodi ya BMMT, na Masheikh wageni waalikwa kwenye Picha ya pamoja wakati wa sherehe za maulid

Sheikh Muhammad Yusuph (Mdiru wa Hawzatu Bilal) akiwasilisha mada wakati wa sherehe za Maulid

Alhajj Abdul Wahid Zakaria (Makamo Mwenyekiti BMMT) akitoa neno la shukrani na kufunga Sherehe