Welcome to Bilal Muslim Mission of Tanzania (Charitable Organization)
CALL US NOW +255 745 111 150
DONATE NOW

SEMINA ELEKEZI KWA MUBALLIGHINA WAPYA

Muballighina wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwa umakini wakati wa semina

Alhamdullillah, kwa neema ya Mwenyezi Mungu Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania (BMMT) ikiwa Hawzatu Bilal, imefanikiwa kuendesha semina elekezi ya siku moja kwa Muballighina wapya ambao wanatarajiwa kuanza kazi kwenye vituo walivyopangiwa haraka iwezekanavyo.

Semina hiyo ililenga kuwapa nasaha Mubalighina juu ya Akhlaq (Tabia njema), kutoa maelekezo juu ya wajibu na majukumu ya Muballighina na namna ya kutekeleza kazi zao za kila siku kulingana na sera na miongozo ya Taasisi.

Semina hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa bodi akiwemo Mwenyekiti wa Bilal Ndugu Hussein Kareem, Makamo Mwenyekiti Alhajj Abdul-Waheed Zakaria, Mwenyekiti wa Bilal kwa vituo vya Pwani na Kusini Ndugu Azizi Hussein, na Mkuu wa Kitengo cha Tabligh Bilal Sheikh Msabaha Mapinda.

Wengine ni Mkuu wa Utawala katika vituo vya Bilal Pwani na Kusini Ndugu Sinani Kamegi, Mdiru wa Hawzatu Bilal Sheikh Muhammad Yusuph, Katibu wa Tabligh (BMMT) Sheikh Abdul – Azizi Atiki na masheikh wengine wa Hawza, pia Semina hii ilipata heshima ya kuwa na masheikh waalikwa ambao ni miongoni mwa masheikh wa mwanzo kabisa wa Bilal na wanafunzi wa Marhoum Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi. Masheikh hao ni Sheikh Ramadhani Kwezi pamoja na Sheikh Hassan Ndimbo.

Semina pia ilijumuisha wazungumzaji wengine akiwemo Msimamizi wa Vituo vya Bilal Mwanza Sheikh Hassan Muhidin aliyeshiriki kwenye semina moja kwa moja kupitia mtandao (Sykpe).

Chini ni picha mbalimbali kutoka kwenye semina hiyo…

Washiriki wa semina wakifuatilia mada (mbashara kutoka Mwanza) kupitia mtandao

Mkuu wa Utawala BMMT Pwani na Kusini Ndugu Sinani Kamegi akiwasilisha jambo kwenye semina

Mwenyekiti wa BMMT Ndugu Hussein Kareem akiwasilisha mada wakati wa semina

(Aliyesimama) Makamo mwenyekiti wa BMMT Alhajj Abdul Wahid Zakaria akiwasilisha mada kwenye semina

Katibu wa Tabligh BMMT Sheikh Abdul – Aziz Atiki akitolea ufafanuzi Manhaj (Sylabus) ya Masomo ya BMMT wakati wa semina

Mwenyekiti wa BMMT Pwani na Kusini Ndugu Aziz Hussein akiwasilisha kwenye semina

Kutoka kulia Sheikh Ramadhani Kwezi, Sheikh Hassan Ndimbo, Sheikh Msabaha Mapinda, Sheikh Muhammad Yusuph na Sheikh Shafi Siraji wakati semina ikiendelea

Washiriki wa Semina kwenye picha ya pamoja baada ya semina