Maasumiin (Watu waliotakasika) hawa ni watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) ambapo wametajwa pia kwenye Qur-an, “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kakutakaseni sana sana”. (33:33).
Mtukufu Mtume Muhammad (s.aw.w) kabla ya kufikwa na umauti ametuasa kushikama na watu wa nyumba yake, pamoja na Qur-an na kwamba vitu hivyo viwili ndio njia ya uongofu.
“Hakika mimi nawaachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, iwapo mtashikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu”. (Rejea: Sahih na Musnad zote).
Hapa tumekuwekea Wasifu (Historia) za Maasumiin wote 14, akiwemo Mtukufu Mtume Muhammad (s.aw.w) mwenyewe kitabu kilichoandikwa na Maulana Sayyid Ali Naqi Saheb na kutarjumiwa na Bwana J.J. Shou na vingine ni vya Hadhrat Fatema (a.s) na maimamu wetu 12 wakianziwa na Imam Ali (a.s) mpaka Imam wa zama zetu Imam Muhammad Mahdi (a.s) vitabu vilivyoandikwa na Dr. M.M. Dungersi na kutarjumiwa na Dr. M.S. Kanju.
Tafadhali bofya link tulizoambatanisha kwenye chapisho hili kupata kitabi husika kwa mfumo wa PDF….
Mtume Muhammad ni miongoni mwa manabii 124,000 walioltumwa na Mwenyezi Mungu (S.W.T) hapa Ulimwenguni ili watu tupate uongofu.
Yeye ndiye wa mwisho katika hao, na ni wa mwisho kati ya wanne waliokuja na vitabu, akija na Qur-an ambayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu mwenyewe.
Mtume Muhammad (s.a.w.w) pia ndie mtume aliyekuja kuukamilisha Uislam, dini iliyoridhiwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya waja wake.
Mwenyezi Mungu anasema, “Leo Nimewakamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na Nimewapendeleeni Islamu iwe dini yenu.” (Qur an – 05:04)
HISTORIA FUPI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1cRvePvArm0Q-FWEL3JQys9hAY6v9NwsN/view?usp=sharing kupakua
Kwa mara ya kwanza kimetoka mnamo mwaka 1979 kikiwa na ISBN NO. 9976 956 533
Huyu ni binti wa Mtume kutoka kwa mke wake wa kwanza, Bi Khadija bint Khuwaylid (r). Baadhi ya riwaya zinamtaja Fatema kama mtoto wa pekee wa Bi Khadija.
Fatema ndie mama wa maimamu kwani kupitia yeye na Imam wa kwanza, Imam Ali (a.s) walipataka maimamu wengine 11.
Mama huyu ni kiigizo cha kila mwanamke, na hiyo ni kutokana na tabia zake na daraja aliyonayo mbele za Mwenyezi Mungu (S.W.T)
WASIFU WA HADHRAT FATIMA (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/10yAWnY4s9WGbnKlr_4I1wUDzqq5GtsyE/view?usp=sharing kupakua
Huyu ni Imam wa kwanza katika mtiririko wa maimamu 12, yeye ndiye baba wa maimam wengine 11. Imam Ali (a.s) ni miongoni mwa wale wa mwanzo kabisa kupata habari za Mtume Muhammad (s.a.w.w) kupewa utume na kumkubali na kumtii Mtume moja kwa moja.
Imam Ali (a.s) amekuwa ni kiungo muhimu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) kutekeleza majukumu yake, na kutokana na hayo ndio akatambulishwa kama “Amirul – Mu’uminin” (Kiongozi wa Wauminini)
Maisha ya Imam Ali (a.s) kwa ujumla ikiwa pamoja na ukaribu wake na Bwana Mtume yanatulazimisha tutake kumjua zaidi Imam ili tujifunze zaidi…
WASIFU WA IMAM ALI (A.S) – Bofya link kupakua
Imam Hassan Al Mujtaba (a.s) ni imam wa pili katika mtiririko wa maimam 12, yeye ndiye mtoto mkubwa wa Imam Ali na Bi Fatma (a.s). Miongoni mwa sifa anazotajwa nazo Imam Hassan ni uchamungu.
WASIFU WA IMAM HASSAN AL MUJITABA (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1MNYg3eTXCZxH8JXXkFuWQfjWZm93bzdH/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM HUSSEIN – SHAHIDU KARBALA (A.S) – Bofya link kupakua
Imam Ali Zainul Abideen (a.s) ni imam wa nne katika mtiririko wa maimam 12, alinusurika kifo katika ardhi ya Karbala kutokana na maradhi aliyokuwa nayo katika wakati wa vita, wakati baba yake Imam Hussien (a.s) na ndugu zake wengine walipouwawa na Yazid Bin Muawiya.
Hata hivyo mpango huu wa Mwenyezi Mungu kwa Imam Zainul Abideen kuugua ilikuwa njia ya yeye kuwa salama na kuwa njia muhimu ya kuendeleza mafundisho ya Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Sehemu kubwa ya maisha imam ilikuwa ni kumuabudu Mwenyezi Mungu, kusujudu na kuomba dua kiasi cha kupewa sifa ya Sajjad (Mwenye kusujudu).
WASIFU WA IMAM ALI ZAINUL ABIDEEN (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1MNYg3eTXCZxH8JXXkFuWQfjWZm93bzdH/view?usp=sharing kupakua
Imam Muhammad Baqir ni imam wa tano katika mtiririko wa maimam 12, Imam Baqir (a.s) anatokana na kizazi cha hashim kutoka pande zote, kwani wazazi wake wanatokana na wajukuu wawili wa Mtume (s.a.w.w) nao ni Hassan na Hussein (a.s).
Miongoni mwa sifa kubwa za Imam ni ukarimu, lakini pia alikuwa na mtaji mkubwa wa elimu.
WASIFU WA IMAM MUHAMMAD BAQIR (A.S) – Bofya link kupakua
WASIFU WA IMAM JA’AFAR SADIQ (A.S) – Bofya link kupakua
WASIFU WA IMAM MUSSA KADHIM (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1FRZHbT-bfR8WBxUz3e_Mll0NewdN6uEM/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM ALI RIDHA (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1yiYQRWpykhnb9lWQVY5gy6O9UmNoysMN/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM MUHAMMAD TAQI (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1J2xHthkSFqXkRoKoz3M9ykgRFruLvgFQ/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM ALI NAQI (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1gRo-nY0BdiI_d05GFAKgFeKQls3X147H/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM HASSAN AL ASKARI (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/1PGgbIljPJxzmo9KM96jMbMBgZx3JKJ_X/view?usp=sharing kupakua
WASIFU WA IMAM MUHAMMAD MAHDI (A.S) – Bofya link https://drive.google.com/file/d/11fWO-4aCwYIlZ9ZeLfBu5KdDF1NpzBM_/view?usp=sharing kupakua